Viulizi

Viulizi

Viulizi hutumika kuulizia mahali, wakati, mtendaji n.k.

 

 

Tunavyo viulizi kama vile.

  • Lini?

Huulizia wakati au muda k.m. Ulifika lini shuleni?

  • Gani?

Huulizia mtendaji au kitendaji k.m. Ni chombo gani kimezama?

 

Muhimu

Kiulizi gani hakichukui kiambishi chochote.

  • pi?

Hutumika sawa na gani? Hata hivyo, kiulizi –pi? huchukua viambishi mbalimbali kulingana na ngeli. K.m. Anatumia kalamu

 

  • ipi?

Anatumia kisu kipi?

Anatumia gari lipi?

 

  • Vipi?

Hutumika katika sehemu mbili:

1.   Kuulizia hali /jinsi/ namna ya jambo k.m Ulifika vipi?


2.     Hutumika kwa kiulizi –pi? katika ngeli ya KI-VI hali ya wingi k.m. Tutatumia vitabu vipi?

 

  • Wapi?

Hutumika kwa njia mbili.

1. Kuulizia mahali k.m. Anaishi wapi?

2. Katika ngeli ya A-WA (wingi) katika kiulizi –pi? k.m. Ni watu wapi waliofika?[resource: 3422, align: left]

 

  • Ngapi?

Huulizia  idadi.  Hutumika tu katika  hali  ya

wingi.  k.m. Ni vitoto  vingapivimefika?

K i u l i z i   – n g a p i   h u c h u k u a   v i a m b i s h i

mbalimbali  kulingana na ngeli?

(Iangalie  sehemu ya kwanza –Ngeli)

 

  • Nani?

Huulizia  mtendaji  k.m. Ni nani anayemlisha mtoto?

   Ni akina nani waliowatumbuiza wageni?

Muhimu

Kiulizi nani ?hutumika katika  ngeli ya (A-WA) pekee.

 

  • Nini?

Hutumika kuulizia kitu au tendo linalotendwa

k.m. Unafanya nini?

 

  • Kwa nini?

Hutumika kuulizia  sababu ya jambo  k.m.

Kwa nini  umechelewa kufika  shuleni?

Kiswahili golden tips sarufi.2b  8/2/12  3:51 PM  Page 44 45

 

  • Aje?

Hutumika kuulizia hali  k.m. Mtoto alianguka aje?

Viulizi: - ngapi na - pi ni viulizi vinavyochukua viambishingeli mbalimbali.

Tazama jedwali lifuatalo:

 

Zoezi

Tumia kiulizi sahihi kisarufi ukamilishe sentensi zifuatazo.

1. Kucheza _____ (kugani, ipi, upi,kupi)  kunakokufurahisha?

2. Maskani _____ (mapi, magani,yapi,ipi) yenye hewa safi?

3. Maiti _____ ( ipi, yapi, yupi,zipi) huzikwa bila sanda?

4. Vitabu vimo mkobani _____ ? ( upi, mpi, ipi, nini)

5. Baba alimtuma _____? ( gani,wepi, nani,upi)

6. Mtachezea uwanjani _____? (upi,ipi, papi,ngapi)

7. Huku ni kwa watu _____ ? ( ngapi, yupi, gani,kupi)

8. Ulitumia jina _____ ? ( jipi, ipi,lipi,ngapi)

9. Nyumba yenu itajengwa _____? (gani, ngapi, ipi, vipi)

10. Mitume _____ ( ngapi,mingapi,wangapi,mangapi) hujulikana duniani?



  • 1 by https://englishlessons4free.wordpress.com/.../speaking-lesson-asking-for-p... used under CC_BY-SA
  • dance by https://en.wikipedia.org/wiki/Performing_arts used under CC_BY-SA
  • ipi_1 by https://medium.com/.../the-pen-cap-that-dreamt-of-becoming-a-pen-e4a04... used under CC_BY-SA
  • kazi by https://en.wikipedia.org/wiki/Agriculture used under CC_BY-SA
  • kisu by https://www.togknives.com/.../TOG%20Knives%20Web%20Brochure%20... used under CC_BY-SA
  • kuanguka by wisgoon.com used under CC_BY-SA
  • kuchelewa by www.nairaland.com/101116/best-primary-schools-lagos used under CC_BY-SA
  • kuondka by www.businesstimes.com.sg/.../vietnam-air-shares-to-start-trading-after-ana... used under CC_BY-SA
  • nani by www.people.com/ used under CC_BY-SA
  • ndege_na_basi by www.allwidewallpapers.com/crown.../Y3Jvd24tZmlyZS1jb2FjaC0xNTAw... used under CC_BY-SA
  • vitabu by www.sjcetpalai.ac.in/library-resources/ used under CC_BY-SA
  • vitotot by https://en.wikipedia.org/wiki/Education used under CC_BY-SA
  • wapi by www.jumeirahgolf-estates.com/.../the-sundials-at-jumeirah-golf-estates-5m... used under CC_BY-SA
  • zama by outdoors360.com/marlin-sinks-fishing-boat-vessel-capsizes-after-hooking-... used under CC_BY-SA
  • 883fc542-7002-4074-8deb-0855491d2964 by elimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.