Vivumishi mseto

- Vipo vivumishi vifuatavyo:

  • Vivumishi visifa k.m. safi, zuri, baya n.k

  • Vivumishi viashiria k.m. huyu, huyo, kile n.k

  • Vivumishi vimilikishi k.m. changu, pako, lake n.k

  • Vivumishi vya kipekee: –ote, –o–ote, –enye, –enyewe, –ngi, –ngine.

Vivumishi visifa

Kuna aina mbili za vivumishi visifa.

  • Vivumishi visifa ambavyo vyanzo havibadiliki k.m.

rahisi, ghali, hodari, kamili, hafifu, halisi, bora, tele, laini, bingwa, stadi, sahihi, maskini, safi, sita, saba, tisa, kumi, haba n.k.

  • Vivumishi visifa ambavyo vyanzo hubadilika kulingana na mizizi ya nomino zinazorejelewa.

Vivumishi hivi hubadilika vyanzo kulingana na ngeli za nomino husika.

Ili kuelewa vyema vyanzo vya visifa hivi, ni vizuri kuzingatia misingi ya ngeli mbalimbali.

Vivumishi viashiria

Kuna aina tatu za vivumishi viashiria
a) Viashiria kawaida.
b) Viashiria radidi.
c) Viashiria visisitizi.

 

Viashiria kawaida | Viashiria vionyeshi

Hivi viashiria hutofautiana kutoka ngeli moja hadi nyingine.

Mifano:- PA - KU - MU.

Karibu - Hapa, huku, humu

Mbali kidogo - Hapo, huko, humo

Mbali - Pale, kule, mle.

Mifano mengine

A - WA - Huyu - huyo, yule
U - I - Huu, huo, ule
U - ZI - Huu, uuo, ule
I - ZI - Hii, hiyo, ile n.k
KI - VI - Hiki, hicho, kile
LI - YA - Hili, hilo, lile

 

Viashiria radidi
- Viashiria hivi hujirudia. Tazama mifano ifuatayo:-
A - WA - Kisiwi huyu huyu, Kisiwi huyo huyo, Kisiwi yule yule.
KI - VI - Kigoda hiki hiki, kigoda hicho hicho, kigoda kile kile.
LI - YA - Magogo haya haya, magogo hayo hayo, magogo yale yale.

 

Viashiria visisitizi
- Hivi viashiria husisitiza nomino.

- Nomino huonyeshwa ndizo zinazozungumzia.

Mfano:-

A - WA - Mwana yuyu huyu, mwana yuyo huyo, mwana yule yule.
KI - VI - Kiko hiki hiki, kiko hicho hicho, kiko kile kile.
U - I - Mkeka uu huu, mkeka uo huo, mkeka ule ule.
LI - YA - Jibu lili hili, jibu lilo hilo, jibu lile lile.

Vivumishi vimilikishi

Mifano:-

Jina lake ni Chamkaro.

Kikapu changu kimejaa matunda.

Pahali pako pamejaa nyuki. n.k

 

Vivumishi vya kipekee

Mifano:- –ote, –o–ote, –enye, –enyewe, –ngi, –ngine.