Mahitaji ya uandishi

Katika shule ya msingi,  mwanafunzi huhitajika kuandika insha mbalimbali. Zipo aina kadhaa za insha ambazo mwanafunzi anatakiwa kuandika.

Ili mwanafunzi aweze kuandika insha hizo vizuri, sharti aelewe na azifuate sheria fulani.

 Mahitaji ya jumla ya uandishi wa insha ni:

  •  Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.

  •  Urefu wa kutosha wa insha.

  •  Lugha sanifu isiyo na makosa ya kisarufi.

  •  Matumizi mazuri ya msamiati.

  •  Upambaji wa lugha kwa kutumia fani mbalimbali kama vile methali, istiara n.k.

  •  Mawazo mazito na yanayotiririka vizuri.

  •  Sentensi fupi fupi zinazoeleweka.

  •  Uzingatiaji wa mada husika.

  •   Kutumia mbinu mbalimbali kama vile taharuki ili kuvutia msomaji wa insha.