Wizara mbalimbali

Wizara ni idara kuu ya serikali inayosimamia na kushughulikia maswala au mambo ya nchi au ya kitaifa kwa kuongozwa na waziri.Wizara mbalili katika nchi yetu.

 • Wizara ya fedha.
 • Wizara ya Elimu, Sayansi and Tecknologia.
 • Wizara ya Mambo ya Nyumbani na Maswala ya Jamii.
 • Wizara ya Barabara na Ujenzi
 • Wizara ya Afya
 • Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni.
 • Wizara ya Utawala wa Mikoa na Usalama wa Taifa.
 • Wizara ya serikali na  Mitaa
 • Wizara ya Kilimo.
 • Wizara ya Habari na Mawasiliano.
 • Wizara ya Mipango na Maendeleo ya Taifa.
 • Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi.
 • Wizara ya Mazingira na Maliasili.
 • Wizara ya Maendeleo ya Ushirika.
 • Wizara ya Maswala ya Jinsia, Michezo,Huduma za Jamii na Utamaduni.
 • Wizara ya Nishati.
 • Wizara ya Uchukuzi.
 • Wizara ya Ustawi wa Maji.
 • Wizara ya Ardhi na Makao.
 • Wizara ya Maendeleo ya Mikoa
 • Wizara ya Turathi za Kitaifa.
 • Wizara ya Biashara na Viwanda.
 • Wizara ya Ushirikiano wa Kanda ya Afrika Mashariki.
 • Wizara  ya Mifungo na Ustawi wa Uvuvi.

Zoezi

1. Ufisadi na uhalifu katika nchi hufaa kudhibitiwa na wizara gani?

2. Haki na ajira za watoto zinafaa kusimamiwa na wizara ipi?

3. Ni wizara ipi inayowajibika kutoa miongozo na kusimamia sera za uadilifu na kuimarisha udugu, uzalendo, ujamaa na mapenzi kati ya jamii nchini?

4. Ni wizara gani inayohusika na utunzaji wa mazingira nchini?

5. Ni wazira gani inayoshughulikia maswala ya wafungwa nchini?

6. Ustawi wa lugha ya Kiswahili kama chombo cha elimu , muungano wa kitaifa na mbinu za maelewano hupaswa kuzingatiwa na wizara gani hasa?

7. Ni wizara ipi au zipi hufaa kusimamia vipindi vya redioni au runinga ili kuhakikisha kuwa havikiuki mipaka ya maadili na kupotosha au kuchafua fikra za jamii hasa kuwapotosha vijana?

8. Shughuli za mahakama zimo katika wizara gani?

9. Wageni wanaoingia nchini hupaswa kuhudumiwa na wizara gani?

10. Chuo za umma na za kibinafsi zinahudumiwa na wizara gani?