Maswali kadirifu

Walemavu

1. Mtu aliye na dosari kwenye viungo vya mwili huitwa _____.

2. Mtu aliyepofuka jicho huitwa _____.

3. Mtu aliyepofuka macho yote mawili huitwa ______.

4. Mtu asiye na meno yote kinywani huitwa ______.

5. Mtu aliye na meno machache kinywani huitwa _____.

6. Mtu aliyezaliwa na meno huitwa _____ au ______.

7. Mtu anayezungumza na ncha ya ulimi huitwa _____ au _____.

8. Mtu aliye katika kidole huitwa _____.

9. Mtu aliyevia huitwa _____.

10. Mwanamke asiyeweza kuzaa huitwa _____.

11. Mwanaume asiyesimika au ambaye jogoo lake haliwiki huitwa _____.

12. Mtu asiye kuwa na rangi kamili ya ngozi huitwa _____.

13. Mtu hasa mtoto anayetabawali kwenye malazi huitwa _____.

14. Mtu aliye na meno yaliyopandana kinywani huitwa _____.

15. Mtu aliyepindika miguu kama uta huitwa _____.