Insha ya methali  by  Lilian Luka

6

Insha ya methali ni insha ya aina gani?

Hii ni insha yenye masimulizi au ufafanuzi wa jambo kwa undani ili kubainisha ukweli wa methali fulani na funzo linalotokana na methali hiyo.

 

Methali nyingi zina maana mbili.

  • Maana iliyo wazi.
  • Maana fiche.

 

Maelekezo kuhusu uandishi huu.

  • Soma swali kisha uwaze maana zote mbili za methali uliyopewa.
  • Orodhesha baadhi ya visa vinavyoweza kufaa.
  • Kuandikiwa insha kwa mujibu wa uelewa wako wa maana ya methali.
  • Teua kisa kimoja kinachoumana zaidi kati ya vile ulivyoorodhesha kisha uandike vidokezi kukihusu.
  • Andika kichwa cha insha ukitumia hiyo methali uliyopewa au sehemu yake ikiwa methali ni refu sana.
  • Andika kichwa chenye maneno ya herufi kubwa yasiyozidi sita.
  • Andika utangulizi wenye mvuto ukizingatia kisa na vidokezo vyako.
  • Tamatisha insha kwa mvuto.

 

Muundo wa kuzingatiwa.

Insha hii ina muundo ulio sawa na ule wa insha yoyote ya masimulizi isipokuwa katika ibara ya kwanza ya utangulizi ambapo maana na matumiziya methali huelezwa.

Mambo yafuatayo yatiliwe maanani

Kichwa

  • Andika kichwa chenye maneno ya herufi kubwa  yasiyozidi sita.
  • Methali uliyopewa ndiyo iwe kichwa,
  • Ikiwa methali ni ndefu sana basi unafaa kuandika sehemu yake ya kwanza pekee kwa mfano, mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya   idi.kichwa cha hii insha chaweza kuwa:
  • MWANA MKAIDI  ama MWANA MKAIDI HAFAI
 

Utangulizi

Anza kwa kueleza maana ya wazi na maana fiche ya hiyo methali katika ibara ya kwanza baadaye unaweza andika methali nyingine moja yenye maana sawa na methali uliyopewa.
 

Mwili

Simulia kisa kitakachodhihirisha ukweli wa methali uliyopewa ukizingatia kanuni zote zinazotawala uandishi wa insha ya masimulizi. Kisa kinachosimuliwa kinafaa kuwa kimoja tu.
 

Hitimisho

Andika mwisho unaosheheneza hatima ya mhusika au wahusika kwa namna inayodhihirisha funzo fulani litokanalo na methali au kisa ulichotoa. Tumia methali hiyo hiyo uliyopewa kuwa kauli ya mwisho kabisa ya insha yako.
 

Zoezi

Andika insha  ya kusisimua ukithibitisha ukweli wa methali hii: Mpanda ngazi hushuka