Maradhi

Aina ya maradhi

Tauni: uele wa homa kali unaosababishwa na viroboto wa panya.

1. Ukimwi: upungufu wa kinga za mwili unaompata mtu aliyeambukizwa na maradhi mengine.

2. Polio/kupooza: ugonjwa wa kuambukiza wa mishipa katika uti wa mgongo unaosababisha kupooza kwa viungo vya mwili na mfumo wote wa neva.

3. Malaria: ugonjwa uletwao na mbu aitwaye anofelesi. Huambatana na homa kali.

4. Kisukari: ugonjwa unaosababishwa na kuzidi kwa sukari mwilini kuliko kipimo kinachohitajika.

5. Pumu: ugonjwa wa mapafu unaomsababishia muwele atatizike anapopumua.

6. Kipindupindu/waba: ugonjwa wa kuhara na kutapika sana. Ni ugonjwa wa kuambukiza.

7. Kichocho: uele wa kukojoa damu unaosababishwa na vidudu vikaavyo katika konokono wanaokaa katika maji baridi yaliyotuama.

8. Kiharusi: uele wa kupooza viungo vya mwili wa mtu na kuwa hisi na nguvu za viungo unatetemesha mwili.

9. Koyo: ugonjwa wa kuvimba miguu kwa mwanamke mjamzito.

10. Kwikwi/kekevu/chechevu: ugonjwa wa kutoa pumzi kinywani kwa nguvu na bila kutarajia.

11. Jongo: ugonjwa wa kuvimba viungo vya mwili na miguu, hasa majira ya mawingu ya mvua.

12. Upele/ukuratu/kaga: ugonjwa unaosababisha vituruturu kuenea mwilini.

13. Kamata: uele unaomshika mtu kwa ghafla.