Viungo vya mwili

Viungo vya mwili

Mwili wa binadamu unavyo viungo tele.

Kila kiungo kina kazi yake na ni lazima vyote vishirikiane ili mwili uwe katika hali nzuri.

1. Ulimi – kiungo cha kuonjea.

2. Meno – hutafunia chakula.

3. Ufizi – nyama iyashikiliayo meno.

4. Utaya – mfupa unaoyashikilia meno.

5. Koromeo/umio – mfereji unaotumikia kuteremshia chakula au kinywaji hadi tumboni. Kifuko kinachotolea mate.

6. Tumbo – sehemu ya kupokea chakula na kuanza kukisaga.

7. Uchanga/uchengele/chango – utumbo mwembamba wa kupitishia chakula kilichosagwa.

8. Moyo/mtima – kiungo kisukumacho damu ili ienee mwilini.

9. Mshipa – mrija au mfereji mdogo unaopitisha damu na pia fahamu katika mwili wa kiumbe.

10. Neva – mishipa ya fahamu mwilini. 11. Ateri– mshipa mkubwa uchukuao damu kutoka moyoni. 12. Pafu – kiungo kinachotumika kusafishia hewa. Hutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi mwilini.

Viungo vya mwili

13. Figo/ buki/nso – kiungo cha umbo la haragwe kisafishacho damu.

14. Ini – kiungo kitiacho nyongo; kiungo kinachobadilisha glukozi kuwa glukojeni; kiungo kinachopima kiwango cha sukari katika damu.

15. Kongosho – kiungo kinachotoa dawa ya kusawazisha damu; kiungo cha kusawazisha sukari kwenye damu.

16. Wengu/bandama– kiungo kitoacho dawa ya kusaidia kusagia protini kwenye chakula.

17. Nyongo – majimaji machungu ambayo hutengenezwa na ini na hutumika kuyeyushia chakula tumboni.

18. Ubongo – sehemu laini kichwani iliyo na mishipa ya fahamu.

19. Fuvu la kichwa – mfupa mgumu ufunikao ubongo.

20. Kibofu – kifuko cha mkojo kilichopo tumboni.

21. Kitefute – mshipa wa shavuni.

22. Kapilari – mishipa midogo ya damu inayosambaa mwilini.

23. Vena – mshipa urejeshao damu moyoni kutoka sehemu mbalimbali za mwili.

Tazama picha hii

Viungo vya mwili

Viungo vya mwili

Viungo vya mwili

Viungo vya mwili

ZOEZI

Zikamilishe methali zifuatazo kwa kutumia majina haya ya viungomwili vya nje: miguu, kisogo, pua, kiganja, shingo, sikio, kinywa, mgongo, mkono, kichwa, viganja, nyonga, nywele, kidevu

1. ___________ ya kuitikiza sio uchungu.

2. ___________ hubeba vyombo, roho hubeba mambo.

3. ___________ kamwambia ndevu kila mtu apataye huwa mwerevu.

4. ___________ jumba la maneno.

5. Masikio hayapiti ___________

6. ___________ la kufa halisikii dawa.

7. Kofi hazilii ila kwa ___________

8. Mpa ___________ si mwenzio.

9. ___________ hayana pazia.

10. Mpiga ngumi ukuta huumiza ___________ wake.

ZOEZI

Zikamilishe methali zifuatazo kwa kutumia majina haya ya viungomwili vya nje: miguu, kisogo, pua, kiganja, shingo, sikio, kinywa, mgongo, mkono, kichwa, viganja, nyonga, nywele, kidevu

11 ___________ mtupu haurambwi.

12. Vita havina ___________.

13. ___________ mmoja haubebi mwana.

14. Mwana hutazama _________ cha nina.

15. Akimbiaye huagana na ____________.

16. ________________ ni shajara.

17. Akili ni______________ kila mtu ana zake.

18. ___________ alichonyia mwana huoshwa hakitatwi.

19. Mtembezi hula ___________ yake.

20. Kata ___________ uunge wajihi. • K.4.35.1 by https://en.wikipedia.org/wiki/Clothing & eLimu used under CC_BY-SA
 • blood_vessels_1 by biology4friends.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • K.4.35.2 by https://www.eyefilm.nl/en & eLimu used under CC_BY-SA
 • viungo_vya_mwili by comet.cls.yale.edu/.../word.asp?... - & eLimu used under CC_BY-SA
 • K.4.35.3 by https://en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • viungo_vya_mwili_2 by https://www.kyliecosmetics.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • K.4.35.4 by https://en.wikipedia.org/wiki/Hand & eLimu used under CC_BY-SA
 • K.4.35.5 by www.famousfootwear.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • K.4.35.6 by unknown & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.