Maeneo ya utawala

- Katika taifa k.v. Kenya, utawala au uongozi huwekwa katika ngazi mbalimbali.

- Tukianzia chini, muundo wa utawala huwa hivi:

  • Kata ndogo – huongozwa na naibu wa chifu.
  • Kata/lokesheni – huongozwa na chifu.
  • Tarafa/divisheni – huongozwa na mkuu wa tarafa.
  • Wilaya/mudiria – huongozwa na mudiri.
  • Mkoa – huongozwa na mkuu wa mkoa (pisii).
  • Taifa – huongozwa na raisi.