Nchi mbalimbali

Duniani kunazo nchi tele.

Kunazo zilizoendelea sana kiuchumi, nyingine zimeendelea kadri ilhali nyingine zimebaki nyuma sana.

 

  •  Nchi zilizoendelea sana kiuchumi huitwa nchi za ulimwengu wa kwanza. Mfano wa nchi hizi ni Marekani, Kanada, Ujapani, na nchi nyingi za magharibi ya bara Ulaya.
  •  Nchi zilizoendelea kadri huitwa nchi za ulimwengu wa pili. Mfano ni nchi nyingi za Asia, Marekani ya Kusini, Australia, Mashariki ya mbali, na mashariki ya kati, kaskazini mwa Afrika na Afrika kusini. Zipo pia nchi za mashariki ya ulaya.
  •  Nchi zilizobaki nyuma sana huitwa nchi za ulimwengu wa tatu. Nyingi za nchi hizi hupatikana barani Afrika kusini mwa jangwa la sahara. Afrika kusini si mojawapo.

Baadhi ya nchi katika kila bara

Bara Ulaya/Uropa

 

Uingereza

Ufaransa

Hispania

Urusi

Lasembagi

Uholanzi

Uyunani

Briteni

Ubelgiji

Ujerumani

Ureno

Uswidi/Swideni

Uswisi

Italia

Ufini

Bara Australia

 

Australia

Visiwa vya Solomoni

Nyuzilandi

Fiji

Papua

Bara Asia

 

Uchina

Bara Hindi

Bahareni

Jordani

Japani

Filipino

Vietinamu

Falme za Kiarabu

Uturuki

Nepali

Siria

Bara Amerika

 

Marekani

Visiwa vya karibiani

Kanada

Ajentina

Kolombia

Visiwa vya Bahama

Brazili

Kuba

Urugwai

Jojia

Meksiko

Peruu

Nikaragwa

Haiti

Jamaika

Bara Afrika

Tafuta nchi mbalimbali katika hii ramani

Kenya

Ginebisau

Nijeri

Jamhuri ya Kongo

Nijeria

Kepuvede

Uhabeshi

Eriteria

Msumbiji

Chadi

Visiwa vya Morisi

Gine

Madagaska (Bukini)

Uswazi

Kameruni

Shelisheli

Aljeria

Senegali

Lesoto

Jibuti

Kodivaa

Misri

Bukinafaso

Moritania

Komoro/

Visiwa vya Ngazija

Zoezi: Jibu maswali yafuatayo.

1. Hapo zamani maharam yalijengwa wapi?

2. Mlima mrefu zaidi barani Afrika u wapi?

3. Ziwa tana hupatikana wapi?

4. Ni kisiwa kipi katika bahari Hindi hukuza karafuu kwa wingi?

5. Yataje mataifa yaliyozitawala nchi hizi enzi za ukoloni? a) Kenya b) Tanzania c) Msumbiji d) Somalia e) Sahara Magharibi.

6. Taja utaifa wa watu wa mataifa yafuatayo: a) Urugwai b) Tanzania c) Uganda d) Ghana e) Zambia f) Togo.