Maswali kadirifu

A. Jaza pengo kwa msamiati sahihi wa malipo.

1. ____ ni pesa za kuingilia kwenye ukumbi wa starehe.

2. ____ ni malipo ya kuvuka daraja au mto.

3. ____ ni malipo ya kusafiri.

4. ____ ni ada alipayo mzazi shuleni mara ya kwanza.

5. ____ ni malipo ya fedha anayopewa mtu aliyestaafu.

B. Toa maelezo kuhusu malipo yafuatayo.

  1. Makadiro
  2. chauchau
  3. uhunzi
  4. pango
  5. kichuo
  6. kiangazamacho
  7. arbuni
  8. bahashishi
  9. mchango
  10. haka

C. Toa majibu sahihi ya maswali yafuatayo.

Chagua kwa haya:

mahari, ruzuku, ada, fungule, mukafaa, mtaji, hiba, kipakasa, sanda, fidia, pango, kilemba, kipunguzo,halasa, machorombozi, mlimbuko, kivusho, nauli, fidia, koto, masurufu, tijara, dafina, kiinuamgongo, kiingilio, kibarua, kodi ya mapato, kifungua mkoba, ridhaa, ushuru.

1. Ahmed alitaka kufundishwa taaluma ya uhunzi. Je alilipa malipo yapi kwa mwalimu wake_______________.

2. Kodi ya nyumba huitwaje?

3. Pesa za adhabu kwa kosa huitwaje?

4. Ni zawadi ipi mtu atoayo kufidia aliyesubiri?

5. Faida itokanayo na biashara huitwaje?

6. Pesa mtu atumiazo kuanzisha biashara huitwaje?

7. Zawadi mtu apewayo kwa kuokota kitu huitwaje?

8. Mali au zawadi apewayo mtu kama ishara ya upendo huitwaje?

9. Mshahara wa wanamaji huitwaje?

10. Malipo kwa daktari huitwaje?

D. Toa majibu sahihi ya maswali yafuatayo. Chagua kwa haya:

mahari, ruzuku, ada, fungule, mukafaa, mtaji, hiba, kipakasa, sanda, fidia, pango, kilemba, kipunguzo,halasa, machorombozi, mlimbuko, kivusho, nauli, fidia, koto, masurufu, tijara, dafina, kiinuamgongo, kiingilio, kibarua, kodi ya mapato, kifungua mkoba, ridhaa, ushuru. 

11. Zawadi apewayo mtu bila kuitarajia huitwaje?

12. Malipo kwa kustaafu huitwaje?

13. Tunaziitaje pesa mtu aliye na deni hupunguziwa baada ya kulipa kiasi fulani?

14. Zawadi atoayo bwana arusi kwa bibi arusi huitwaje?

15. Malipo zaidi ya mshahara wapewayo wafanyikazi kutokana na faida iliyopatikana huitwaje?

16. Pesa mtu apewazo mfiwa kumsaidia kwa mazishi huitwaje?

17. Malipo ya kwanza ya daktari huitwaje?

18. Malipo ya kuingilia ukumbini mwa sinema huitwaje?

19. Malipo ya kuvukia daraja huitwaje?

21. Malipo kwa kazi yoyote ya mkono huitwaje?

22. Malipo kwa kazi ya kutwa au ya makataa huitwaje?

23. Malipo ya kuolea huitwaje?

24. Malipo ya kuingizia bidhaa nchini ni ?

25. Malipo kwa serikali kulingana na mapato ya mtu huitwaje?

26. Malipo kwa kusababishiwa hasara au maumivu huitwaje?

27. Malipo kwa kuharibiwa sifa huitwaje?

28. Malipo ya kujiunga na chuo cha elimu ni?

29. Malipo ya kusafiria ni?

30. Malipo yatolewayo na serikali kwa idara mbalimbali kugharamia mahitaji ni?

20. Pesa za matumizi nyumbani au safarini huitwaje?