Malipo

- Malipo pia huitwa ada. Malipo hutolewa kutokana na shughuli mbalimbali.

 

1. Karo: Ada ya shule inayotolewa na mwanafunzi.

2. Nauli: Malipo ya kusafiria.

3. Koto: Ada ya kumwingiza au kumsajili mwanafunzi shuleni.

4. Mahari: Malipo ya kuolea.

5. Fidia: Malipo kwa kusababishiwa hasara au maumivu.

6. Ridhaa: Malipo kwa ajili ya kuharibiwa sifa au jina.

7. Riba: Malipo kwa mkopo.

8. Pensheni: Malipo ya kustaafu (kiinuamgongo)

9. Arbuni: Malipo ya kwanza ya kununulia kitu/malipo ya kufungia kitu kisinunuliwe na mwengine.

10. Masurufu: Pesa za matumizi safarini au nyumbani.

 

11. Kiangazamacho: Zawadi kwa kuokota kitu kilichopotea.

12. Kodi ya mapato: Malipo kwa serikali kulingana na mapato ya mtu.

13. Ushuru wa forodha: Malipo kwa serikali kwa ajili ya kuuza au kuingiza bidhaa nchini.

14. Dia/arshi: Malipo kwa ajili ya kutolewa damu.

15. Kiingilio: Ada ya kuingilia michezoni.

16. Kivusho: Ada kwa ajili ya kutumia daraja au pantoni kuvukia.

17. Mapoza: Malipo kwa mtu aliyeudhiwa ili kutuliza hasira zake.

18. Kilemba: Malipo apewayo mhunzi na mwanafunzi wake baada ya kuhitimu mafunzo.

19. Tuzo: Zawadi apewayo mtu kwa kufanya jambo zuri.

20. Faini: Pesa za adhabu kwa kosa.

 


21. Dhamana: Fedha zitolewazo na mshtakiwa ili kuachiliwa kitambo kesi yake ikatwe.

22. Karisaji/ ajari/ovataimu: Malipo ya pesa kwa muda wa ziada wa kufanya kazi.

23. Mrabaha: Malipo anayopewa mwandishi na kampuni iliyotoa kazi yake kila baada ya muda fulani wa mauzo.

24. Mchango: Malipo ya hiari ili kufanya shughuli fulani k.v. ujenzi wa shule.

25. Karadha: Mkopo usiotozwa riba.

26. Mshahara: Malipo ya mfanyikazi ya kila mwezi kwa kazi alioajiriwa.

27. Marupurupu: Malipo alipwayo mtu zaidi ya yale ya kawaida.

28. Ujira: Malipo kwa kazi iliyofanywa.

29. Fungule: Malipo kwa daktari.

30. Bahashishi: Zawadi kwa utumizi bora au huduma bora za kazi.

 

 31. Kiokozi/kombozi: Malipo ya kukombolea kitu kilichotekwa nyara au kunyakuliwa.

32. Urithi: Mali yaachwayo na hayati na kupewa mtu fulani.

33. Rehani: Malipo ya kitu kilichowekwa dhamana ili kikombolewe baadaye.

34. Pango: Kodi ya nyumba au chumba anayolipa mpangaji kila mwezi au baada ya muda fulani.

35. Honoraria: malipo/ pesa kama bakshishi kwa kufanya kazi maalum.