Rangi

Rangi ni ule ubainifu au ujuaji wa miale ya mwangaza inapoingia katika kitu fulani.

Kunazo rangi za kila aina

Mifano

 • nyeusi
 • nili
 • nyeupe
 • hudhurungi/kahawia
 • manjano
 • rangi ya dhahabu (zari)
 • samawati/samawi
 • nyekundu
 • kijani kibichi
 • zambarau mbivu
 • rangi ya fedha
 • kijivu
 • buluu
 • rangi ya machungwa

Aina za Rangi.

A. Teua majibu sahihi kwa maswali yafuatayo

1. Rangi ya damu ni ________.

2. Majani yasiyokauka yana rangi ya ______.

3. Rangi ya mvi ni ______.

4. Rangi ya makaa ni ______.

5. Chai ya mkandaa huwa na rangi ya ___.

6. Zitaje rangi za upinde kuanzia juu hadi chini.

7. Mpingo una rangi ipi?

8. Rangi ya mbingu isiyo na mawingu ni ______.

9. Zabibu mbivu huwa na rangi ipi?

10. Gololi ya jicho huwa na rangi ipi?

11. Rangi ya mboni ya jicho ni ______.

12. Rangi ya samli ni ______.

13. Rangi ya bafta ni ______.

14. Kwa kawaida kiungo cha bizari huwa narangi ipi?

15. Thaluji huwa na rangi ipi?

B. Taja vitu mbalimbali vilivyo na rangi zifuatazo.

1. Manjano

2. Machungwa

3. Maji ya kunde

4. Dhahabu

5. Nyeusi.