Vikembe

 - Vikembe Pia huitwa vizawa. Ni wana wa viumbe mbalimbali.

 

Mifano;

 •  Malaika - Mtoto wa binadamu.

 •  Ndama - Mtoto wa ng’ombe, ndovu.

 •  Buu - Mtoto wa nzi.

 •  Funutu/maige/kimatu/tunutu - Mtoto wa nzige.

 •  Jana/chana – Mtoto wa nyuki.

 •  Kifaranga – Mtoto wa kuku.

 •  Kinda – mtoto wa ndege/nyuni.

 •  Shibli – Mtoto wa simba.

 •  Kinegwe – Mtoto wa papa.

 •  Kiluwiluwi – Mtoto wa chura, mbu.

 •  Kiwavi – Mtoto wa kipepeo.

 •  Kitungulekituju – Mtoto wa sungura.

 •  Kihongwe – Mtoto wa punda.

 •  King’onyo – Mtoto wa mdudu.
 •  Kisuse – Mtoto wa nge.

 •  Kingo – Mtoto wa jicho
 •  Mjoli – Mtoto wa mtumwa
 •  Kilebu – Mtoto wa mbwa/kelbu.

 •  Kivinimbi – Mtoto wa nguruwe.

 •  Chengo – Mtoto wa nyangumi.

 •  Kinyaunyau – Mtoto wa paka.

 •  Kibuli – Mtoto wa mbuzi.

 •  Nyumbu – Mtoto kati ya punda na farasi.

 •  Chotara/hafukasti/suriama/shombe – mtoto kati ya wazazi wa rangi mbalimbali.
 •  Saraka/athiari/jarari/dawati – mtoto wa meza.