Utangulizi

Mnyama ni kiumbe ambacho kina uhai wala sio mtu, mdudu au mmea. Kuna wanyama wanaokaa nyumbani (mifugo) na wanaoishi kichakani (wanyamapori). Mifugo huwekwa kwa minajili ya pato kwa binadamu. Wanyamapori pia ni kivutio kikubwa sana kwa watalii.

Kwa hivyo basi, wanyama wote wanastahili kutunzwa na kuhifadhiwa vilivyo.