Maumbile ya nchi

Maumbile ya nchi ni kama vile:

 • Mto: Bonde lenye maji yanayotiririka wakati wote.
 • Ziwa: Sehemu yenye maji mengi iliyozungukwa na nchi kavu.
 • Bahari: Eneo kubwa la maji ya chumvi linalozungukwa na nchi kavu.
 • Upwa: Sehemu ya pwani ambayo maji hujaa na hupwa.
 • Delta: Sehemu mto unapojigawaganya vipande viwili au zaidi unapoingia baharini.
 • Kinamasi: Mahali penye tope au telezi.
 • Chemchemi: Mahali maji yanapobubujika.
 • Gema/genge/korongo: mteremko mkali kwenye kingo za mto.
 • Kisiwa: Eneo la nchi kavu lililozungukwa na maji.
 • Msitu: Eneo kubwa lililo na miti mingi.
 • Nyika: Sehemu inayoota nyasi na miti midogo.
 • Jangwa: Eneo kubwa na kame ambalo kwa kawaida huwa na mchanga lisiloota nyasi wala miti.

 

 • TambarareNchi isiyokuwa na miinuko wala mabonde.
 • Bonde: Sehemu ya ardhi iliyo katikati ya vilima viwili.
 • Mlima: Sehemu ya ardhi iliyoinuka juu sana kuliko sehemu nyingine.
 • Nguu: Sehemu ya juu kabisa ya mlima.
 • Volkano: Mlipuko mkali wa moto unaotokea ndani ya dunia kumwaga zaha ambayo mara nyingi husababisha milima katika uso wa dunia.
 • Kreta: Sehemu inayopatikana juu ya mlima. kifungulima:
 • Kisima cha jangwani. Kisiwa: Eneo la nchi kavu lililozungukwa na maji.
 • Wangwa: Sehemu ya pwani iliyo na mikoko ambapo maji hujaa na kupwa.
 • Ghuba: Sehemu kubwa ya bahari iliyoingia ndani ya pwani.
 • Mgodi: Mahali palipochimbuliwa madini.
 • Jabali: Mwamba mkubwa.
 • Kituka: Mahali penye miti mifupimifupi iliyoshonana na nyasi.

 

Zoezi:

Jibu maswali yafuatayo kikamilifu.

Tumia maneono haya. chemichemi, wangwa, tambarare, ziwa, nguu, kisiwa, upwa, migodi, kinamasi, msitu, gema, mto, nyika, jangwa, zilizala, delta

1. Mahali penye miti tele mikubwa kwa midogo, nyasi kwa vichaka ni _________.

2. Eneo kame ambalo halina nyasi wala miti ila mchanga ni _________.

3. Sehemu iliyo na nyasi na miti midogo ni _________.

4. Kilele cha mlima ni _________.

5. Eneo lenye maji mengi ambalo limezungukwa na nchi kavu ni _________.

6. Eneo la nchi kavu ambalo limezungukwa na maji huitwa _________.

7. Bonde lililo na maji yanayotiririka kila wakati hususan kuanzia mlimani kuelekea maeneo ya chini ni _________.

8. Mahali ambapo maji ya mto yanaanguka kwa kima kirefu toka juu ya mwamba ni _________.

 9. Sehemu mto unapojigawa pande mbili au zaidi uingiapo baharini ni _________.

10. Sehemu ya nchi iliyoloa maji na imejaa tope na utelezi ni _________.

11. Kisima cha jangwani ni _________.

12. Mahali maji yanapobubujika ni _________.

13. Sehemu ya pwani ambapo maji hujaa na kupwa ni _________.

14. Pwani palipo na mikoko na mchanga pasipofikwa maji mafu _________.

15. Sehemu ya kuchimbwa madini ni _________.

16. Sehemu isiyo na milima wala mabonde ni _________.