Maliasili ya taifa

Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile.

Mifano: misitu, maji, madini n.k.

Aghalabu, maliasili ya nchi huchangia katika utajiri wa nchi husika k.m.

Afrika kusini imenawiri kiuchumi kutokana na utajiri wa madini.

ZOEZI Jibu maswali yafuatayo.

1. Madini yatumikayo kukatia vioo huitwa ______________.

2. Madini yatumiwayo kutengenezea mapambo ya fahari k.v. pete huitwa ______________.

3. Madini magumu yatumiwayo kukata vyuma huitwa ______________.

4. Madini majimaji yenye rangi ya fedha yatumiwayo katika themometa huitwa?

5. Madini meupe yatumiwayo sana kupaka juu ya chuma kuzuia kutu?

6. Madini ya chumvi chungu yatumiwayo kutengenezea sabuni ni ______________.

7. Unga mweupe upakwao kuta za nyumba ni ______________.

8. Madini ya rangi nyekundu yanayong’aa baada ya kusuguliwa na hutengenezea nyaya za umeme ni ______________.

9. Madini meupe yachimbwayo ardhini na hutumika kutengenezea vioo na ng’amba za sanaa ni ______________.

10. Madini ya buluu na kijivu hafifu ambayo huyeyuka rahisi ikichomwa ni ______________.