Maswali kadirifu

A. Andika katika nambari.

Subui zidisha robo
Thumni tano
Sudusi sita
robo
thuluthi si sawa na robo
tusui saba

Akisami 5/10 husomwa _____ ( tano juu ya kumi, ushuri tano )

B. Jibu maswali yafuatayo.

1. Katika darasa la nane, kulikuwa na wanafunzi thelathini. Iwapo humusi nne walikuwa mabenati, je maghulamu walikuwa wangapi?

2. Musa alitumia robo ya mshahara wake kwa kodi ya nyumba. Thuluthi ya msha•hara uliobakia alitumia kwa mavazi na uliosalia akaweka akiba. Je, iwapo mshahara wake ulikuwa shilingi elfu moja na mia mbili, aliweka akiba ya pesa ngapi?

3. Katika mkutano wa chifu, wanawake hamsini walihudhuria. Ikiwa idadi ya wanaume iliyohudhuria ilikuwa maradu•fu ya ile ya wanawake, je mkutano ulihudhuriwa na watu wangapi kwa jumla?

4. Juma ana pipi kumi naye Fatuma ana pipi nane. Pipi za Hamisi ni nusu ya zile za Juma, Pipi za Maria ni robo tatu ya zile za Fatuma. Je, wote wanne wana idadi ipi ya pipi?

5. Mzee Maisha ana umri wa miaka sabini na mitano. Naye Kazana mtoto wake, ana umri humusi tatu wa ule wa babaye. Je Kazana ana umri upi? 

6. Sitini na nne ukizidisha kwa thumni ni ngapi?

7. Baada ya kupiga miguu kwa kilomita sita, Musa aligundua kuwa alikuwa ametembea thuluthi ya safari yake. Je, safari yake ilikuwa ya umbali wa kilomita ngapi?

8. Mnamo mwezi wa Aprili, seremala alitumia humusi mbili ya mwezi katika karakana yake. Je, alitumia siku ngapi nje ya karakana?

9. Robo karne ni sawa na miaka mingapi?

10. Humusi mbili ni sawa na asilimia ngapi?

11. Sufuri nukta sita ni sawa na asilimia _______.

 

C. Zipange aksami zifuatazo kuanzia ndogo hadi kubwa.

  • thuluthi mbili
  • humusi tatu
  • ushuri
  • thumni tano
  • subui tano
  • ushuri tatu
  • tusui mbili
  • sudusi tano
  • robo tatu
  • humusi mbili
  • kumi na moja
  • kumi na nne

 

D. Andika kwa maneno

a) miche 601, 234

b) maembe 265

c) nyumba 7, 301, 828

d) ng’ombe 5, 386

e) viti 63

f) minyoo 3

g) mifugo 86, 002

h) kusoma 4

i) sokoni pale 5

j) viroboto 21