Tarakimu

- Tarakimu ni alama ya hesabu ionyeshayo idadi.

- Tarakimu huanzia sufuri na huendelea hadi matrilioni.

- Kwa sasa, trilioni ndicho kiwango cha juu zaidi cha tarakimu.

 

Mifano ya tarakimu:

  • 0 - sufuri
  • 10 -  kumi

 

  • 100 - mia moja.

  • 1000 - elfu moja.

10,000 - elfu kumi.

  • 100,000 - elfu mia moja. (Laki moja.)

  • 200,000 - laki mbili
  • 300,000 - laki tatu
  • 400,000 - laki nne
  • 500,000 - laki tano, nusu milioni.
  • 1,000,000 - milioni moja.

  • 10,000,000 - milioni kumi.

  • 100,000,000 - milioni mia moja.

 

  • 4 - nne.
  • 15 - kumi na tano.
  • 104 - mia moja na nne.
  • 115 - mia moja na kumi na tano.
  • 1, 005 - elfu moja na tano.
  • 2, 016 - elfu mbili na kumi na sita.
  • 4, 103 - elfu nne, mia moja na tatu. 
  • 5, 229 - elfu tano, mia mbili ishirini na tisa.
  • 10, 006 - kumi elfu na sita.
  • 20, 022 - ishirini elfu, na ishirini na mbili.
  • 30, 919 - elfu thelathini, mia tisa kumi na tisa.
  • 100, 009 - laki moja na tisa.

 

  • 200, 036 laki mbili na thelathini na sita.
  • 500, 916 laki tano, mia tisa kumi na sita
  • 607, 024 laki sita, elfu saba na ishirini na nne.
  • 729, 687 laki saba, ishirini na tisa elfu, mia sita themanini na saba.
  • 1, 000, 008 milioni moja na nane.
  • 2, 000, 061 milioni mbili sitini na moja.
  • 4, 000, 296 milioni nne , mia mbili tisini na sita.
  • 6, 007, 380 milioni sita, elfu saba, mia tatu themanini
  • 7, 096, 319 milioni saba, tisini na sita elfu, mia tatu kumi na tisa.
  • 9, 918, 401 milioni tisa, laki tisa kumi na nane elfu, mia nne na moja.

 

Nambari shufwa

Hizi ni tarakimu ambazo idadi yazo inagawanyika kwa mbili sawasawa. k.m. 2, 6, 8,10, 12, 14, 18, 20, 22, 24, 26, 28,30, 32 n.k.

Nambari witiri

Hizi ni tarakimu ambazo idadi yazo haigawanyiki kwa mbili sawasawa k.m. 1, 3, 9, 15, 21, 25, 27 n.k.

Nambari tasa

Namba isiyoweza kugawanyika kwa nambari nyingine yoyote isipokuwa yenyewe na moja. k.m. 1, 3, 5, 7, 11, 13, 17, 19, 23, 29, 31, 37 n.k.

Asilimia

Asilimia (huandikwa %) huonyesha “kwa kila mia moja.” k.m. 10% - Asilimia kumi. 20.7% - Asilimia ishirini nukta saba.

 



  • elfu_kumi by www.banknotes.com/ug.htm & eLimu used under CC_BY-SA
  • elfu_mia_moja by https://zimbabwedollars.net/.../zimbabwe-100-thousand-dollar-banknote & eLimu used under CC_BY-SA
  • Elfu_moja by http://www.techweez.com/2015/01/05/airtel-africa-new-top-level-appointments/ & eLimu used under CC_BY-SA
  • KenyanCoins by worldcoingallery.com/countries/circ_sets/Kenya.html & eLimu used under CC_BY-SA
  • Kumi by www.clipartpanda.com/categories/open-hands-clipart-black-and-white & eLimu used under CC_BY-SA
  • Mia_moja by www.theeagora.com/evolution-of-currency-in-kenya/ eLimu used under CC_BY-SA
  • Milioni by moneymarketsea.blogspot.com/2010_10_01_archive.html & eLimu used under CC_BY-SA
  • Milioni_kumi by www.kachwanya.com/2015/03/23/safaricom-competitions/ & eLimu used under CC_BY-SA
  • Zimbabwe by https://en.wikipedia.org/wiki/Hyperinflation_in_Zimbabwe & eLimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.