Jikoni

- Jikoni ni mahali mwa upishi.

- Jikoni munaweza kuwa katika shule, nyumba au hata katika hoteli.

 

Msamiati wa jikoni

  • Jiko – chombo cha kupikia. Jiko linaweza kuwa la makaa, kuni, stima, mvuke, gesi na hata la jua.
  • Seredani – jiko la makaa.
  • Mafiga/mafya – mawe matatu ya jiko la kuni.
  • Dohani – mfereji wa kutolea moshi jikoni. 


 Aina za jiko


  •  Uchaga – sehemu ya kuwekea kuni.

  • Karo – sehemu ya jikoni ya kuoshea vyombo.
  • Mwiku/kiporo/ bariyo/uporo – chakula kilicholala mpaka asubuhi.
  • Ukoko – mabaki/ masazi ya chakula yanayoganda kwenye chombo kilichopikia chakula hicho.
  • Staftahi – kifunguakinywa
  • Kisabeho – chakula cha asubuhi.
  • Kishuka/ chamcha – maakuli ya adhuhuri
  • Kilalio/chajio – chakula cha jioni
  • Masizi – unga mweusi wa makaa au moshi ambao aghalabu hupatikana kwenye sufuria au chungu cha kupikia.

 

  • Utandu – masalio yaliyomwagika chakula kinapopikwa.
  • Viungo – vitu vinavyotia chakula ladha au harufu nzuri k.m. chumvi, kitunguu, iliki, karafuu, masala, bizari, tui,
  • Mlale – Utandabui mweusi utokanao na moshi jikoni.
  • Chungu – chombo cha kupikia.
  • Kata – chombo cha kuchotea maji mtungini.
  • Mbuzi – chombo cha kukunia nazi.
  • Susu – chombo cha kuwekea sahani au chungu.
  • Mwiko – kifaa cha kupakulia, kusongea au kukorogea chakula.
  • Buli/birika – chombo cha kutilia chai au kinywaji kingine.
  • Kinu – chombo cha kusagia nafaka, viungo n.k.
  • Kikaango – chombo kinachotumiwa kukaangia vyakula k.v. chapati au mayai.
  • Kifumbu/kunguto,kichujio – chombo cha miyaa cha kuchujia nazi.

  •  Kikamulio – kifaa cha kukamulia matunda ili kuyatoa maji yake.
  • Deste – Sahani kubwa ya kuwekea halua.
  • Degi – sufuria kubwa ya kupikia chakula kingi.
  • Sinia – sahani kubwa ya mviringo itengenezwayo kwa madini – hutumika kupakulia chakula.
  • Chano/fua – sinia kubwa ya ubao ya kupakulia chakula.
  • Tanuri – jiko la kuokea mikate.
  • Jokofu/friji/ jirafu – chombo mfano wa kabati chenye mtambo wa kuleta baridi na kuhifadhi aghaabu vyakula.
  • Kihoro – sahani ya mti.

 

Vitendo jikoni

  • Kukoka moto – Asha moto. 
  • Kupuliza moto – Kusababisha moto uwake kwa nguvu zaidi.
  • Kuzima moto – kupoesha moto. 
  • Kuteleka/ kuinjika – kuweka chungu juu ya jiko.
  • Kuepua – kuondoa chungu juu ya jiko. 
  • Kutokosa – kuchemka Kutokota – chemka kwa nguvu.
  • Kupepeta – rusharusha nafaka katika ungo kuondoa makapi



  • K.4.12.1 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
  • 202da9e7-4499-433f-8e63-a850b13d0b63 by elimu used under CC_BY-SA
  • 2a1f9a1a-3d3a-491c-a5cc-726ff4ec904c by elimu used under CC_BY-SA
  • 6506649e-35ff-4878-af98-135be12dbd45 by elimu used under CC_BY-SA
  • dde8eb53-526e-443c-84bb-bc5abadb6dda by www.findinglife.ca & eLimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.