Makao

Makao ni mahali kiumbe huishi.

Makao ya wavulana waliotiwa jando ni kumbi.

Rais huishi kwenye ikulu.

Mfalme huishi kwenye kasri.

Mtawala huishi kwenye kitala.

Mfungwa hukaa gerezani/husuni.

Makao ya mtu angojeaye kesi ikatwe ni mahabusi/mahabusu/rumande.

Ng’ombe huishi kwenye zizi/chaa/zeriba/ buruji.

Samaki huishi majini

Kasuku huishi kwenye tundu.

 

Kuku huishi kwenye kizimba.

Fuko huishi shimoni.

Nyuni huishi kiotani.

Makao ya kiwavi ni kifukofuko.

Makao ya panzi ni nyasini.

Konokono huishi kwenye koa/kombe

Funza huishi vidoleni.

Mchwa huishi katika kichuguu/kidurusi/ kingulima/kishirazi.

Jana huishi katika masegasega.

Nyuki huishi katika mzinga.

Buibui huishi kwenye utando/utandabui.

Makao ya uchango ni utumbo.

 

Jibu maswali yafuatayo.

1. Ng’ombe huishi __________ naye konokono huishi __________.

2. Makao ya ng’onzi ni _____________.

3. Nyuni huishi ______ naye kuku hukaa ________.

4. Funza huishi __________.

5. Samaki huishi ______ naye sungura huishi ______.

6. Makao ya nyuki ni _____ nayo makao ya kasuku ni ________.

7. Mahabusu hukaa ________ naye mshukiwa hukaa ________.

8. Makao ya mfalme ni ________ na yale ya rais ni _______.

9. Buibui huishi kwenye ______ naye jana (mtoto wa nyuki) huishi kwenye ________.

10. Makao ya mchwa ni _______ nayo ya mbuzi ni ________.