Nomino za makundi

- Nomino za makundi hutumika kuonyeshea mkusanyiko wa nomino au nauni nyingi.

- Nomino za makundi zinaweza kuwa za viumbe k.v. watu au vitu k.v. magari.

Mifano: Kaumu ya watu

 • Halaiki ya watu
 • Umati wa watu
 • Hadhara ya watu
 • Sisisi ya watu
 • Sufufu ya watu
 • Msafara wa watu
 • Kigaro cha askari, jeshi la askari
 • Kikoa cha waimbaji/wachezaji

Mifano:

 • Mkururo wa watoto

 • Jopo la waandishi
 • Baraza la wazee
 • Genge la vibarua/wezi
 • Mzengwe wa wagomaji

 • Jamii ya watu/miti/vifaranga
 • Msitu wa miti

 • Mlolongo wa magari, watu

 • Kipeto cha barua
 • Safu ya watu/milima/nyumba
 • Kicha cha mboga, funguo
 • Kilinge cha wachawi

Mifano:

 • Thurea ya nyota

 • Pakacha la matunda (kikapuni)
 • Kichala cha matunda (mtini)
 • Kifungu cha matunda (sokoni), viazi, ndizi, sukumawiki
 • Kikonyo cha zabibu
 • Tita la nguo, kuni
 • Mzinga wa nyuki
 • Bumba la nyuki
 • Bumba la majani
 • Bumba la tumbaku, bumba la nyuki

Mifano:

 • Biwi la takataka, kwekwe, magugu, simanzi
 • Jaa la takataka, magugu, kwekwe
 • Funda la maji
 • Chemichemi ya maji.
 • Jozi ya viatu

 • Jozi ya soksi, karata, vipuli
 • Wingu la moshi, vumbi, nzige
 • Shada la maua

 • Mtungo wa maua
 • Koja la maua, mawaridi
 • Chane la ndizi, nafaka

 • Mkungu wa ndizi
 • Chano la ng’ombe

Mifano:

 • Hombo la samaki
 • Mtungo wa samaki
 • Tumbi la samaki
 • Hombo la samaki

 • Doti la leso, kanga
 • Bunda la noti, karatasi
 • Shungi/tuta la nywele
 • Sharafa la ndevu
 • Seti ya sahani, vikombe, fanicha
 • Shuke la nafaka
 • Shazi la nafaka
 • Halmashauri ya shule
 • Baraza la mawaziri

Mifano:

 • Tanuri la chokaa
 • Tonge/donge la ugali
 • Tone la damu
 • Kifurushi cha nguo
 • Karne ya miaka
 • Korija ya shanga, blanketi
 • Kundi la fisi, ndege
 • Topa la vitabu

 • Mnofu wa nyama
 • Paneli ya majaji

Mifano:

 • Misitu ya miti
 • Kanzi la maharagwe, mahindi, ngano, mpunga
 • Kichaka cha miti
 • Robota la pamba
 • Korija la magunia/mablanketi/vitambaa
 • Jora la bafta/vitambaa/vitenge
 • Kopo la uji/chai/kahawa
 • Darzeni ya mayai/matunda/vikombe

Zoezi A: 

Tumia nomino za makundi sahihi kati ya haya kujaza mapengo vipeto, hombo, madonge, matopa, majora, minofu, jumuia, mashunge, matuta, tita. 

1. Mama alinunua ______ la samani.

2. Wasasi waligawana ____ ya nyama.

3. Msomi huyo alikuwa na _____ ya vitabu.

4. Tarishi alibeba _____ vya barua.

5. Shambani kulionekana ____ ya udongo.

6. Nilimwona mjakazi aliyebeba ____ la kuni.

7. Washonaji walinunua ____ ya vitambaa.

8. Jitu hilo lilibugia ____ ya sima.

9. Tuliyakata ____ ya mpunga.

10. Viongozi wa _____ ya madola walikutana jijini.

ZOEZI B

Tumia majibu mwafaka kujaza mapengo.

1. Mnamo msimu wa kiangazi mawingu ya __________ yalionekana angani.

2. Tuliliona ______ la ng’ombe huko malishoni.

3. Wakati wa usiku ______ za nyota zilionekana mbinguni.

4. Mrembo huyo alikuwa na ______ ya vipuli ndeweni.

5. ______ la mawaziri lilikutania huko ikulu.

6. Wezi hao walitiwa mbaroni wakiwa na ______ vya nguo vya wenyewe.

7. Mchuuzi huyo alibeba ________ ya mayai.

8. Seremala yule alinitengenezea _______ ya fanicha ya kifahari.

9. _______ hilo la takataka lilinuka fee!

10. Akina mama hao walitunukiwa ____ ya leso.

 

11. Kijana huyo alijuta aliporushia _______ wa nyuki mawe.

12. Wachapishaji walikuwa na ________ ya karatasi.

13. Barabarani kulionekana ________ wa magari.

14. __________ cha wachawi kulifumaniwa huko mwituni kikipanga njama.

15. ________ la waandishi lilikutana kurati•bu mikakati ya uandishi.

16. Mwanamke huyo alikuwa na _________ la nywele la kupendeza.

17. Tuliyameza __________ ya maji ili kukatia kiu.

18. _________ cha askari kilifika kuzima ghasia za wagomaji.

19. Muthoni ameteuliwa kwa ____ ya shule.

20. Shangazi Nyokabi atanunua ________ ya sahani. • umati by https://www.crowdrise.com/rebuildingthevillage & eLimu used under CC_BY-SA
 • misitu-ya-miti by www.geograph.ie/photo & eLimu used under CC_BY-SA
 • mkururo-wa-watoto by allafrica.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • mlolongo-wa-magari by www.geograph.ie/photo & eLimu used under CC_BY-SA
 • mzengwe-wa-wagomaji by tuko.co.ke & eLimu used under CC_BY-SA
 • thurea-ya-nyota by phys.org › Astronomy & Space › Astronomy & eLimu used under CC_BY-SA
 • chane-la-ndizi by https://wall.alphacoders.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • jozi-ya-viatu by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • shada-la-maua by www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • hombo-la-samaki by nourishtheplanet.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • topa-la-vitabu by www.thinkinclusive.us & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.