Visawe

Haya ni maneno yaliyo na maana sawa au yanayokaribiana sana kimaana | kwa maana.

mtu – mja, adinasi, mahuluki, insi, binadamu.

rafiki – msena, mwandani, bui, muhibu, sahibu

adui – hasimu

baba – abu

mama – nina

msichana – banati, gashi

mvulana – mvuli, ghulamu

soko – chete, gulio

nyumbani – kiamboni, mastakimuni, chengoni

Furaha – faraja, bashasha, naima, ucheshi

Hasira – mafutu, kero, hamaki, ghadhabu

Lengo – dhamira, nia, azma, kusudi, gharadhi, tarajio, tumaini, matilaba

Tajiri – mkwasi, mlalaheri

Maskini –mlalahoi, fukara, hawinde, mkata, fakiri.

Pesa – njenje, ngwenje, fedha, hela

Uzembe – uvivu, ajizi

maringo – madaha, madaha

uso – wajihi

mke – ahali

familia – aila, mlango

barabara – tariki, gurufa, baraste

ugonjwa – maradhi, ndwele

hongo – rushwa, chai, chirimiri, chauchau, kadhongo, chichiri, mvugulio

mwizi – luja, mkupuzi, pwagu, pwaguzi

Jela – gereza, husuni

afya – siha, udole

jitimai- huzuni, kihoro, simanzi

Fujo – ghasia, zogo, zahama

Ukuta – kiambaza

Usingizi – ndezi, gonezi,

Kazi – amali, gange

Mavazi – lebasi

Mtoto – mkembe

Makamu – naibu

Kitanda-Samadari

Moyo – mtima,  fuadi

Kijiji – kitongoji, kaya, karia

 Fanicha – samani

Ndoa – nikahi, nikaha, arusi

Ndoto – ruiya, njozi

 

ZOEZI A.

Tumia neno jingine lenye maana sawa na lililoandikwa kwa wino uliokolea. hayawani, chudi, njozi, matatizo, ugani, wahaka, nilihama, wanalandana, zawadi, kurunzi, ngeu, aushini, soka.

 1. Mtoto huyu alikuwa na bidii kupita kiasi.
 2. Askari alitumia tochi kumulikia.
 3. Usiku huo nilipata ndoto ya ajabu.
 4. Maishani mwangu sijalaza damu.
 5. Masaibu yaliponizidia, niligura mjini.
 6. Wanafunzi walicheza kandanda huku uwanjani.
 7. Niliingiwa na wasiwasi m wenzangu alipokosa kufika.
 8. Huko msituni, tulimwona mnyama wa ajabu.
 9. Ndugu hao wanafanana kama Kurwa na Doto.
 10. Aliposhinda, alipata tuzo.

Andika visawe viwili vya kila neno lifuatalo:

a) mpagazi     b) msichana       c) adabu         d) duni

e) makao        f) huzuni            g) afya           h) aibu

i) moyo           j) mwizi            k) busara        l) kasoro

m) kimatu       n) cheo             p) shamba       q) umri

r) bingwa        s) dalili             t) dhiki            u) fikiri

 

Andika visawe zaidi ya moja kwa kila neno lifuatalo:

a) konde   b) chemchemi    c) nderemo       d) ngedere  e) ibada  

f) daawa       g) ijara         h) umahiri       i) masaibu  j) gombo

k) ngamizi    l) shauku     m) ndwele       n) kibali     p) panka       

q) kambarau  r) siha        s) kuzimu         t) nikaha     u) pululu

v) mlozi         w) mkwasi        x) mwele     y) mwangazi • banati by Midas touch used under CC_BY-SA
 • nyumbani by Home Dzine used under CC_BY-SA
 • rafiki by Global giving used under CC_BY-SA
 • soko by move bubble used under CC_BY-SA
 • waya by pinterest used under CC_BY-SA
 • malaika by eLimu used under CC_BY-SA
 • nina by Elimu used under CC_BY-SA
 • furaha by Public enemy Africa used under CC_BY-SA
 • maskini by eLimu used under CC_BY-SA
 • moyo_1 by Various sources used under CC_BY-SA
 • mtoto by pinterest used under CC_BY-SA
 • mvivu by dreamstime used under CC_BY-SA
 • pesa by pinterest used under CC_BY-SA
 • aila by eLimu used under CC_BY-SA
 • bara by Tuko.co.ke used under CC_BY-SA
 • jela by eLimu used under CC_BY-SA
 • kipusa2 by Midas touch used under CC_BY-SA
 • kitanda by bfd used under CC_BY-SA
 • Harusi by Spirit of black Paris used under CC_BY-SA
 • kijiji by Joke used under CC_BY-SA
 • moyo by Various sources used under CC_BY-SA
 • samani by eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.