Maswali kadirifu

A.Toa maana ya pili ya kitawe

 

1. Ninamjua koo, kuku jike aliyekomaa; pia kuna koo ______.

2. Bibi ni nyanya. Aidha, bibi ni ______.

3. Taka ni sawa na uchafu. Vilevile, taka ni _____.

4. Shinda ni kubaki pahali kutwa nzima. Shinda pia ni ______.

5.Pesa ni sawa na fedhaFedha vile vile ni ______

 6. Haya ni kiashiria. Haya ni sawa na _____.

7. Ninamjua kaa samaki. Pia kuna kaa ____.

8. Taa ni kile kifaa cha kutolea mwangaza. Taa pia ni _____.

9. Ninamjua mbuzi mnyama afuguaye nyumbani. Mbuzi pia ni ______.

10. Kupata ndoto usingizini ni otaOta pia ni ______.

 

B. Toa maana ya pili ya kitawe.

 

11. Mwezi ni kile kipindi cha takribani siku thelathini. Mwezi pia ni ____.

12. Ninamjua buibui mdudu mwenye miguu minane. Buibui pia ni _____.

13. Koma ni alama ya uakifishaji. Vilevile, koma ni _____.

14. Nyumba ni sawa na makao. Vilevile nyumba ni __________.

15. Kamba ni uzi mrefu wa kufungia vitu kama vile mizigo. Kamba pia ni ______.

16. Ua ni kitendo cha kutoa uhai. Ua pia ni _____.

17. Paa ni kitendo cha kwenda juu angani. Paa vilevile ni _____.

18. Chai ni kinywaji cha kuburudisha. Chai pia ni ______.

19. Sita ni tarakimu. Sita pia ni _______.

20. Kipo kiunganishi piaPia halikadhalika ni ______.

C. Toa maana ya pili ya kitawe.

 

21. Paka ni mnyama wa nyumbani jamii ya chui. Paka aidha ni ______.

22. Panda ni kuweka mbegu ardhini ili ziote. Panda pia ni ______.

23. Ziwa ni eneo kubwa la maji lililozungukwa na nchi kavu. Aidha ziwa ni ____.

24. Mkahawa ni sawa na hoteli. Mkahawa pia ni ____.

25. Zama ni sawa na kale. Zama halikadhalika ni ______.

26. Kikuku ni pambo la mkononi. Pia kuna kikuku ______.

27. Pango ni uwazi mkubwa ulioko katika ardhi. Pango vilevile ni _______.

28. Panga ni kukaa nyumba au chumba, kwa malipo. Panga pia ni ______.

29. Chungu ni siokuwa tamu. Chungu pia ni ______.

30. Mpaka ni mahali ambapo ni kikomo cha kitu na kingine. Aidha, mpaka ni _______.

 

D: Taja vitawe vya maelezo yafuatayo.

shika, kiboko, chuma, pamba, kitovu, kifaru, tai, kifungo, baa, mori, kanda, mada, kopa, bali, konde.

 

1. Ni sufi ya mmea iliyo nyeupe na laini. Chakula au masurufu ya wakati wa safari.

2. Kuchukua fedha au kitu kinachouzwa na kuahidi kulipa baadaye. Chapa ya umbo kama moyo.

3. Jambo au kitu kiletacho hasara. Mahali panapouzwa na kunywewa pombe.

4. Ni kovu lililoko katikati ya tumbo. Ni kituo kikuu cha shughuli fulani.

5. Ni kiini cha habari au jambo linalozungumziwa. Ni hali ya kushikilia jambo liendelee.

6. Ni kiunganishi kisawe cha lakini. Ni pambo la sikioni.

7. Ni adhabu ya mtu kuwekwa gerezani. Ni kitu kinachotumiwa kufungia vazi.

8. Madini ngumu inayotumiwa kujengea na kuundia vitu. Fanya kazi kama vile biashara na kupata faida.

9. Ni shamba lililolimwa. Ni vidole vya mkono vilivyofumbwa yaani ngumi.

10. Ni mtu asiyeweza kuaminika. Ni malipo yanayotolewa kwa mganga.

 

11. Ni ndege mkubwa mwenye makucha marefu ambaye aghalabu hula mizoga. Ni kitambaa kilichotengenezwa maalu•mu kwa kuvaliwa kwenye ukosi.

12. Ni kitendo cha kuteremka kutoka mahali juu. Ni leso au kitambaa kikubwa.

13. Ni sawa na hasira. Ni ng’ombe jike ambaye bado hajazaa.

14. Ni mnyama mkubwa mnene anayeishi katika maji baridi. Fimbo ya kupigia.

15. Ni gari la chuma la kivita lenye mzinga. Ni mnyama mkubwa mwenye kipusa usoni.