Vitawe

Haya ni maneno ambayo yana maana zaidi ya moja.

 • Kibibi -tamko la heshima la kumwita mtoto msichana. -aina ya andazi.

 • Koo -sehemu ya mwili. -kuku wa kike aliyekomaa. -familia.

 • Mbuzi -Mnyama wa kufugwa. -kifaa cha kukunia nazi.

 • Tai -Ndege mla mzoga. -ukosi wa blausi au shati. - aina ya vazi.

 • Tembo -Pombe. -Ndovu.

 • Kata -eneo la utawala/lokesheni. -kutenganisha kitu kwa chombo k.v. kisu. -kifaa cha kuchotea maji mtungini.

 • Meza -Kupitisha chakula kooni hadi tumboni. -kifaa cha kuandalia mlo.

 • Chupa -Kuruka. -Chombo cha kutilia vinywaji k.v. maji.

 • Kima -Mnyama jamii ya nyani. -Nyama iliyosagwa.

Pia -Kiunganishi. -umbo.

 •  Tembe -kuku mdogo wa kike. -kidogo k.v. dawa. -nyumba fupi ya udongo isiyo paa ila dari lililotengenezwa kwa udongo.

 • Shuka -Leso. -Teremka.

 • Hema -Kibanda cha turubali/ chandaru. -Tokwa na pumzi kwa nguvu.

 • Nyanya -Mamaye wazazi wangu. -Aina ya mboga.

 • Karia -Kijiji/kaya. -kiti cha pili cha baiskeli cha kubebea mtu wa pili au kubebea mizigo. -sehemu ya juu ya gari ya kubebea mizigo.

 •  Gofu -Mabaki ya jengo lililobomoka. -Mchezo wa magongo.

 • Ala -Mfuko wa kuwekea kisu au upanga. -Neno la kuonyesha mshangao. -Zana ya kufanyia kazi.

 • Taa -Chombo cha kutolea mwangaza. -Samaki mkubwa mwenye umbo bapa na mkia mrefu. -Nidhamu.

 • Amba – sema/eleza. - neno la kukubali jambo. - Pengine,labda. - Kiwakilishi.

 • Ambo – ugonjwa ueneao. - kitu kama gundi kinachonata.

 • Bui -Buibui mkubwa. -Rafiki. -Mchezo wa watoto.

 • Buku -Panya mkubwa. -kitabu kilichopigwa chapa.

 • Mto -Mtaro wenye maji yanayotiririka wakati wote. -mfuko ulio na pamba.

 • Mlango -Uwazi wa kuingilia k.v. nyumba. -Familia. -sehemu ya kitabu, sura.

 •  Chale -Aina ya samaki wa baharini. -Aina ya pambo. -Kidudu cha baharini chenye sumu. -Mtu anayefanya mambo ya kuchekesha.

 •  Changa -Kitu kisichokomaa. -Toa kitu k.v. fedha ili kukusanya kwa lengo fulani.

 • Kama -mithili. -bana/kaba.

 •  Ndege -eropleni. -nyuni.

 • Jana -mtoto wa nyuki. -siku kabla ya leo.

 • shinda -isiyojaa. -kaa mahali kutwa nzima. -fanikiwa.

Zoezi A: Toa maana ya pili ya kitawe

1. Ninamjua koo, kuku jike aliyekomaa; pia kuna koo ______.

2. Bibi ni nyanya. Aidha, bibi ni ______.

3. Taka ni sawa na uchafu. Vilevile, taka ni _____.

4. Shinda ni kubaki pahali kutwa nzima. Shinda pia ni ______.

5.Pesa ni sawa na fedha. Fedha vile vile ni ______

 6. Haya ni kiashiria. Haya ni sawa na _____.

7. Ninamjua kaa samaki. Pia kuna kaa ____.

8. Taa ni kile kifaa cha kutolea mwangaza. Taa pia ni _____.

9. Ninamjua mbuzi mnyama afuguaye nyumbani. Mbuzi pia ni ______.

10. Kupata ndoto usingizini ni ota. Ota pia ni ______.

 

Zoezi B: Toa maana ya pili ya kitawe.

11. Mwezi ni kile kipindi cha takribani siku thelathini. Mwezi pia ni ____.

12. Ninamjua buibui mdudu mwenye miguu minane. Buibui pia ni _____.

13. Koma ni alama ya uakifishaji. Vilevile, koma ni _____.

14. Nyumba ni sawa na makao. Vilevile nyumba ni __________.

15. Kamba ni uzi mrefu wa kufungia vitu kama vile mizigo. Kamba pia ni ______.

16. Ua ni kitendo cha kutoa uhai. Ua pia ni _____.

17. Paa ni kitendo cha kwenda juu angani. Paa vilevile ni _____.

18. Chai ni kinywaji cha kuburudisha. Chai pia ni ______.

19. Sita ni tarakimu. Sita pia ni _______.

20. Kipo kiunganishi pia. Pia halikadhalika ni ______.

 

Zoezi C: Toa maana ya pili ya kitawe.

21. Paka ni mnyama wa nyumbani jamii ya chui. Paka aidha ni ______.

22. Panda ni kuweka mbegu ardhini ili ziote. Panda pia ni ______.

23. Ziwa ni eneo kubwa la maji lililozungukwa na nchi kavu. Aidha ziwa ni ____.

24. Mkahawa ni sawa na hoteli. Mkahawa pia ni ____.

25. Zama ni sawa na kale. Zama halikadhalika ni ______.

26. Kikuku ni pambo la mkononi. Pia kuna kikuku ______.

27. Pango ni uwazi mkubwa ulioko katika ardhi. Pango vilevile ni _______.

28. Panga ni kukaa nyumba au chumba, kwa malipo. Panga pia ni ______.

29. Chungu ni siokuwa tamu. Chungu pia ni ______.

30. Mpaka ni mahali ambapo ni kikomo cha kitu na kingine. Aidha, mpaka ni _______.

 

Zoezi D: Taja vitawe vya maelezo yafuatayo. shika, kiboko, chuma, pamba, kitovu, kifaru, tai, kifungo, baa, mori, kanda, mada, kopa, bali, konde.

1. Ni sufi ya mmea iliyo nyeupe na laini. Chakula au masurufu ya wakati wa safari.

2. Kuchukua fedha au kitu kinachouzwa na kuahidi kulipa baadaye. Chapa ya umbo kama moyo.

3. Jambo au kitu kiletacho hasara. Mahali panapouzwa na kunywewa pombe.

4. Ni kovu lililoko katikati ya tumbo. Ni kituo kikuu cha shughuli fulani.

5. Ni kiini cha habari au jambo linalozungumziwa. Ni hali ya kushikilia jambo liendelee.

6. Ni kiunganishi kisawe cha lakini. Ni pambo la sikioni.

7. Ni adhabu ya mtu kuwekwa gerezani. Ni kitu kinachotumiwa kufungia vazi.

 

Taja vitawe vya maelezo yafuatayo. shika, kiboko, chuma, pamba, kitovu, kifaru, tai, kifungo, baa, mori, kanda, mada, kopa, bali, konde.

8. Madini ngumu inayotumiwa kujengea na kuundia vitu. Fanya kazi kama vile biashara na kupata faida.

9. Ni shamba lililolimwa. Ni vidole vya mkono vilivyofumbwa yaani ngumi.

10. Ni mtu asiyeweza kuaminika. Ni malipo yanayotolewa kwa mganga.

11. Ni ndege mkubwa mwenye makucha marefu ambaye aghalabu hula mizoga. Ni kitambaa kilichotengenezwa maalu•mu kwa kuvaliwa kwenye ukosi.

12. Ni kitendo cha kuteremka kutoka mahali juu. Ni leso au kitambaa kikubwa.

13. Ni sawa na hasira. Ni ng’ombe jike ambaye bado hajazaa.

14. Ni mnyama mkubwa mnene anayeishi katika maji baridi. Fimbo ya kupigia.

15. Ni gari la chuma la kivita lenye mzinga. Ni mnyama mkubwa mwenye kipusa usoni. • kata_1 by Missouri business used under CC_BY-SA
 • kata_2 by eLimu used under CC_BY-SA
 • kata_3 by Neatly coiled used under CC_BY-SA
 • kata_4 by The bay used under CC_BY-SA
 • kibibi_2 by Tim in Kenya used under CC_BY-SA
 • Kibibi by cloudmind used under CC_BY-SA
 • koo_1 by Zadyball used under CC_BY-SA
 • koo_2 by pinterest used under CC_BY-SA
 • koo_3 by Mail Online used under CC_BY-SA
 • mbuzi_1 by eLimu used under CC_BY-SA
 • mbuzi_2 by Bright blue eyes used under CC_BY-SA
 • tai_1 by qtbird used under CC_BY-SA
 • tai_2 by About neckties used under CC_BY-SA
 • tembo_1 by Simba Nia's blog used under CC_BY-SA
 • chupa_1 by Felice Cohen used under CC_BY-SA
 • chupa_2 by Nice clip art used under CC_BY-SA
 • kima_1 by Public Domain Pictures used under CC_BY-SA
 • kima_2 by Non Veggies used under CC_BY-SA
 • meza_1 by Living wilderness used under CC_BY-SA
 • meza_2 by iFurn used under CC_BY-SA
 • Pia by Racked used under CC_BY-SA
 • shuka_1 by The Chive used under CC_BY-SA
 • shuka_2 by Various sources used under CC_BY-SA
 • tembe_1 by Robert's ranch used under CC_BY-SA
 • tembe_2 by Nailtip.net used under CC_BY-SA
 • tembe_3 by Beta news used under CC_BY-SA
 • tembe_4 by Daily Nation used under CC_BY-SA
 • ala_2 by Sellfast used under CC_BY-SA
 • ala by Grey knives used under CC_BY-SA
 • gofu by Various sources used under CC_BY-SA
 • hema by Various sources used under CC_BY-SA
 • Image-29_nyanya by Various sources used under CC_BY-SA
 • karia_1 by Daily Trust used under CC_BY-SA
 • karia_2 by pinterest used under CC_BY-SA
 • Taa by Various sources used under CC_BY-SA
 • amba by pinterest used under CC_BY-SA
 • Ambo by Various sources used under CC_BY-SA
 • Bui by Various sources used under CC_BY-SA
 • Buku by Various sources used under CC_BY-SA
 • Image-40_mto by Various sources used under CC_BY-SA
 • mlango by Various sources used under CC_BY-SA
 • chale by Various sources used under CC_BY-SA
 • changa_1 by Various sources used under CC_BY-SA
 • Image-45_kama by Daily Kos used under CC_BY-SA
 • jana by pinterest used under CC_BY-SA
 • Kama_1 by The Hindu used under CC_BY-SA
 • Kama_2 by Blood of Jesus ministries used under CC_BY-SA
 • Ndege_2 by Various sources used under CC_BY-SA
 • shinda by The Kenyan weekly post used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.