Majira

Majira ni kipindi kirefu kiasi cha wakati.  

Aghalabu kipindi hiki huwa na hali fulani ya hewa.

Masika/kifuku: Majira ya mvua tele ya mfululizo.

Kiangazi/ukame: Majira ya jua kali.

Vuli/mchoo: Majira ya mvua ndogondogo ambazo hupatikana wakati wa pepo za kaskazi.

Kipupwe: majira ya baridi. Matlai: msimu wa pepo zinazovuma kutoka mashariki.

 

Zoezi A:Jibu maswali yafuatayo vilivyo

Msimu wa mvua nyingi huitwa?_________
Kishuka huliwa wakati wa?____________
Kiporo huliwa lini? _______________
Jua huchwa lini? _________________