Dira

- Dira ni chombo mfano wa saa.

 

- Dira ni chombo cha kuwaelekeza wasafiri katika pande za Dunia.

- Huwa na mshale uzungukao wenyewe.

- Hutumiwa kuonyeshea mwelekeo na hata majira.

- Dira huwa na pande nne kuu.

- Nazo ni kaskazini, mashariki, kusini na magharibi.

 

- Mbali na pande hizi nne, kunazo pande nyingine.

- Tazama dira ifuatayo, pande a - h hutamkwa vifuatavyo;

 

1) Kaskazini

2) Kaskazini kaskazini mashariki

3) Kaskazini mashariki

4)  Mashariki kaskizini mashariki

5) Mashariki

6) Mashariki kusini mashariki

7) Kusini mashariki

8) Kusini kusini mashariki

9) Kusini

10) Kusini kusini magharibi

11) Kusini magharibi

12) Magharibi kusini magharibi

13) Magharibi

14) Magharibi kaskazini magharibi

15) Kaskazini magharibi

16) Kaskazini kaskazini magharibi

 

 

Ili kukumbuka kwa urahisi dhania kuwa unasema,

“Kaskazini ya kaskazini mashariki kaskazini ya kaskazini mashariki n.k”

  • Jua huchomoza upande wa mashariki na hutua/huzama upande wa magharibi.
  • Jua linapochomoza twasema Kumekucha au Kumepambazuka au mawio.
  • Ni vizuri kuelewa uhusiano wa upande wa jua, wakati na upande wa kivuli k.v: Asubuhi Jua huwa upande wa mashariki. Kivuli huwa upande wa magharibi.
  • Alasiri Jua huwa upande wa magharibi. Kivuli huwa upande wa mashariki.
  • Jua linapotua au linapozama husemwa kumekuchwa au kumekutwa. Wakati huo ni machweo au machwa au magharibi.
  • Kaskazini ndio utosi wa dira. Yaani dira huanzia Kaskazini.
  • Jina jingine la Kaskazini ni Shimali au Shemali na Matlahi ni jina lingine la Mashariki.
  • Jua huwa mkabala na kivuli, yaani iwapo jua li kusini, kivuli kitakuwa kaskazini.